Breaking News

Njoo Tupeane Mbinu Za kuwakwepa Vibaka

Sehemu nyingi nilizoishi ni uswazi, nitakachokwambia hapa ni uzoefu wa moja kwa moja kipindi cha utoto niliwahi kua kwenye kundi lililojiita Majani Unit (halipo tena hili kundi) lilikua na wanamuziki, vibaka, dancers na wapenda ugomvi.

Ukiwa kama mtembezi wa usiku unakua unajihatarisha kukutana na vibaka (siyo majambazi) lakini kuishi kwangu maeneo mbali mbali sijawahi kukabwa ingawa ni mtembezi mzuri tu wa usiku, ili kupunguza asilimia za kukabwa kuna mbinu zinaweza kukusaidia.

La muhimu ni kujitahidi kupunguza kumvutia kibaka akukabe, mvuto wa kukaba unaupunguza kwa kufanya haya.

1. Jinsi Unavyotembea
Mwendo wa kutompa mori kibaka akukabe ni ule wa kujiamini hatua ziwe ndefu lakini zisiwe za kuonesha kua una hamu ya kulipita eneo hilo kwa haraka. Usijitanue lakini onesha kua show ikianza hapa mtashindwa nyinyi.
Hua natembea nikiwa nimenyooka, macho yanatazama mbele na kuacha mikono iyumbe ila kiukakamavu.

2. Mavazi na Accesories zake
Usivae mavazi kama unaenda kufanya shooting halafu ni usiku, unatafutia watu dhambi. Wala nguo isiwe na nembo ambayo inaonekana dhahiri, hata viatu visiwe vya kutamanisha. Kama ni simu epuka kuitumia ikiwa na mwanga mkali au usiitumie kabisa.
Nashauri vaa pensi na shati/ vest haswa hizi vest za siku hizi zinakua kubwa kushinda mwili wa mhusika.

3. Kama unavuta sigara au bangi, tembea huku ukivuta. Kama hauvuti nunua kimoja wapo ukiwa unatembea onekana kama unavuta, ila unaweza kukutana na sungusungu ukiwa na bangi hivyo jipange kwa majibu pia.

4. Jinsi unavyoongea. Kama ukiongea una lafudhi zinazoonekana ni za kinyonge huku sauti yako ikiwa haina uzito wowote nashauri usitembee kabisa usiku.

Mfano hayo yote yamefanyika na bado vibaka wakakufuata?
Naassume haumiliki bunduki, pia naassume hauna mazoezi ya ngumi, nashauri onesha kua hautaki ugomvi na unataka suluhu hivyo ukisalimiwa itika, ukisimamishwa simama, jibu utakachoulizwa.

Jua kwamba dakika 1 kwenye ugomvi ni nyingi sana zikizidi na huna mazoezi pumzi itakuishia utaaibika, Ikiwa ugomvi utaanza tumia sekunde 30 za kwanza vizuri kwa kurusha ngumi jichoni, kutumia mawe, kutumia kichwa (kichwa piga kuanzia usawa wa pua kuja chini mdomoni), au teke la korodani.

Sekunde 30 zinazofuata ni za wewe kutoka mbio, mbio kama vile maisha yako yameshikiliwa na hizo mbio (ndiyo maana nikasema vaa pensi na vesti).

Mwisho wa yote epuka kuzurura na mwanamke usiku, hua wanatia uzito sana, na pia ni aibu kukimbia mbele ya mwanamke.

Lete mbinu zako mdau.

0 Comments

Type and hit Enter to search

Close