Inakuaje wadau wa mazoezini?
Wakati mwingine unajikuta unakosa pesa ya kuingia gym hivyo unajikuta huna option zaidi ya kukaa nyumbani ukiangalia ulivyoviingiza kwa wiki sita vikipukutika.
Lakini kwa muda nimekua nikitumia njia ambayo inanifanya kuubakisha mwili kwa kuujaza na kuukata.
Best of all, hili zoezi unaweza ukafanya popote na ndani ya dakika 45 (kutegemea na unavyotaka kua challenged).
Ili kuyafikia malengo ya hapo inabidi tufanye haya mazoezi kwa kutumia mtindo unaoitwa Tabata Protocol.
Zoezi tutakalolifanya litakua ni push ups (pushapu).
Na kanuni yetu itakua;
Zoezi moja litajumuisha seti nne.
Seti moja itajumuisha reps 20.
Kupumzika kati ya seti na seti ni sekunde 10.
Kupumzika kati ya zoezi moja na jingine ni dakika moja.
Anza na Pushap za Kawaida.
Hii ni ile aina ya pushap ambayo watu wengi wameizoea. Kama alizopiga Magufuli ila wewe usikunje ngumi.
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi moja tunaenda jingine.
Pushap za miguu ikiwa imeinuka.
Mimi hua naweka miguu kitandani, unaweza ukaiweka kwenye stuli, jiwe au hata ndoo ukiigeuza juu chini. Pale daraja la Manzese miguu hua inawekwa kwenye ngazi.
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi la pili, tunaenda jingine.
Tunakuja na Spartan Pushap.
Mikono yako inatakiwa ipishane, mmoja uwe mbele kushinda mwingine. Lakini ukiwa unaenda juu mkono uliokua mbele utaurudisha nyuma na uliokua nyuma unaupeleka mbele.
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi la tatu tunaenda jingine.
Tunamalizia na Pushap za Magoti kugusa Chini.
Unaweka mikono kama unataka kupiga pushap alizopiga Magufuli, ila magoti yako yatakua yamegusa chini na usikunje ngumi kama Magufuli.
Utaanza kwa kwenda juu ukishuka chini hiyo ni moja, utafanya hivyo mara 20. Utapumzika sekunde 10 na kurudia tena mara nne.
Hapo tunakua tumemaliza zoezi letu.
NB.
-Utavuja sana jasho ndani ya dakika moja
-Kama hujawahi kufanya mazoezi, usifanye spartan pushap na hii ya magoti kugusa chini kwa sasa mpaka utakapozoea. Pia punguza idadi ya seti na reps, jiongezee na muda wa kupumzika.
-Natumia uzoefu na kujifunza kwa wengine, sijasomea, ushauri wangu siyo wa kidaktari.
-Comment workout yako tupate kujifunza zaidi.
0 Comments