Kwanini uvae nguo za ndani zilizo na makalio ya upepo, wakati una nguvu na wewe bado kijana, kwanini uangaike kununua madawa ya kichina yalio na madhara kemkem katika afya yako. Najua wachache wana uwezo wa kufanya upasuaji kwa kuweka maumbile mengine (plastic surgery) lakini pia sio salama.
Kupata mwili kama wa Nick minaj, inawezekana kwa kujituma hasa kwa mazoezi, mazoezi aina ya squat ni mazoezi ambayo yanaweza kukufanya ukawa na shape ya kupendeza kama utafanya kwa kufwata maelekezo na kuzingatia kanuni za mazoezi hayo.
Squat haikusaidii tu kutengeneza shape kama makalio pekeake ila pia husaidia kushape miguu yako, kusaidia kutoka minyama uzembe au (cellulite), mazoezi haya yanaweza ambatana na mazoezi ya kupunguza tumbo na kushape kiuno chako ili uwe na kiuno kama nyigu yaani chembamba.
Nini cha kufanya? Kwa wale wasio na uwezo wa kuwatafuta wataalamu wa mazoezi haya au kwenda Gym, kuwa pamoja nasi hapa unaweza ukafanya ukiwa nyumba iwe na vifaa au bilaa vifaa.
Matokeo baada ya kufanya mazoezi haya yanatokana na juhudi zako na najua watu wengi ni wavivu na wanatamani matokeo ya haraka kitu ambacho hakiwezi kuwa raisi. Unaweza kutumia zaidi ya miezi mitatu kupata unachokifanyia kazi kwa bidii. Jiwekee ratiba yako ya mazoezi kwa dakika 15 tu kila siku na unaweza kuona matokeo.
Unaweza pia kufanya kama ni tamaduni yako kukimbia na kufanya mazoezi mengine ya mwili kwani huwezi kutengeneza tu shape kama huna afya nzuri hii nikiwa na maana ukiwa mfanya mazoezi zingatia mlo wako na kunywa maji mengi, matunda na mboga za majani. Jenga shepu yako na mazoezi na sio madawa.
Hivi karibuni blog yako ya mazoezini itkuletea mpango mzima wa mazoezi kwaajili ya shepu na afya yako
1 Comments
ReplyDeleteKutana na mtaalamu WA mitishamba dr toka tanga anazo dawa za uzazi ..ugumba...kukuza hips shape na makalio..kukuza uume na kunenepesha...anatibu bawasiri . Kupata watoto mapacha UTI sugu...mpigie kupitia 0744903557 dawa zake ni mitishamba na anasafirisha popote ulipo Kwa anayehitaj