Breaking News

Hatua za mwanzo za kufahamu kuhusu Meditation.

Watu mbalimbali wamekuwa wakianza kupata ufahamu juu ya meditation na wengine tayari wameshaanza kujifunza kufanya kitendo kicho. Meditation ni kitedo cha muhimu kwani kina faida kubwa na wengi waliojitolea muda wao kujifunza meditation (mfano mimi), wamenufaika na meditation. Nimeona nielezee katika post hii na ninaamini itawasaidia wengi wambao wangependa kujua. 
***

Kwanza kabisa, kabla ya kufanya meditation ni kufahamu lengo la meditation ni nini, ni muhimu ukafahamu akili ni nini, inafanyaje kazi, energy zinazomzunguka mtu, utambue vyema baadhi ya maelezo ambayo yatasaidia mtu kujua uelewa kidogo kuhusu meditation. Kutambua hivyo itakusaidia kufahamu jinsi meditation inavyofanya kazi katika ufahamu. 

Tukianza na sababu ya meditationa ni kuweza kufahamu akili yako inavyofanya kazi, kujiepusha na mateso/shida ndogondogo, huepusha hasira, hukupa uwezo mkubwa wa kuwa m'bunifu mfano kama wewe ni mchoraji, mwanamuziki n.k, inakusaidia kuwa na maamuzi sahihi katika maisha yako. Na kama utaweza kuwa na maamuzi mazuri katika choices mbalimbali katika maisha itakusaidia sana kwani msingi wa maisha ni choices tunazoweka kila siku na kila saa. Ukishaweka nia sahihi juu ya meditation kinachofuata ni kufahamu nini kinatakiwa kiwepo kabla ya kufanya meditation. Pia katika imani nyingine kama Wahindi na Wabudha, viongozi wao wa imani wanapata nguvu ya kiimani, ufahamu na wanafunuliwa jicho la tatu kupitia meditation. Hata sayansi nayo inaamini Enlightenment inaweza kutokea katika meditation na kumfanya mtu afunguke kiimani. Meditation inabadili mpaka DNA na kumpa mtu enlightenment (Ipo siku nitaelezea experience/hali ya enlightenment inakuwaje). 



Kuandaa Sehemu ya Meditation.

Andaa sehemu nzuri na maalum ambayo utakuwa unafanya meditation. Mfano inaweza ikawa chumbani unapolala, chagua sehemu au eneo ambalo utakaa chini vyema bila usumbufu, penye hewa nzuri na safi (fresh air), penye hali ya hewa cool au ya kawaida. Ni vyema kuchagua sehemu ambayo hauitumii kwa shughuli nyingine au mfano ukiwa haupiti sana eneo hilo au huweki vitu unavyotumia eneo hilo. Ni kwa sababu itapunguza kuwazawaza pale utakapokuwa unataka kunyamazisha akili, inaepeusha kumbukumbu za eneo hilo kuja wakati wa meditation, pia ni vyema kwani meditation ni kama sala, ni kitendo kisafi hivyo ni vyema eneo la kufanyia sala na meditation kuwekwa katika hali nzuri. 
Ukishachagua eneo unaweza ukaweka vitabu vyako vya imani katika eneo hilo, inategemeana na imani yako. Halafu ukishamaliza kinachofuatia tafuta mto wa kukalia ambapo utaukalia. Tafuta mto mzuri ambao ukiukalia hautaumia (kwani utakuwa unakaa kwa muda mrefu). Halafu tafuta nguo za kuvaa ambazo hazibani na zilizo comfortable. Chagua wakati maalumu ambao utakuwa unameditate. Ni vyema kutumia dakika 20 na kuendelea katika kumeditate. Pia meditate kila unapoamka na kila kabla ya kulala. Baadaye utakapoweza kumeditate vyema utaweza hata kumeditate kwa dakika moja katika kila lisaa. 

Ukishajianda hivyo kinachofuatia ni kukaa na kumeditate. 




Huo ni mkao mzuri katika meditation kwani una faida zifuatazo. 

Unakusaidia damu kuzunguka maeneo ya juu ambapo ndipo sehemu zenye umuhimu katika meditation, zinasababisha energy kutoka kwenye dunia kupitia kwenye uti wa mgongo na kukupa utulivu wakati wa meditation, pose linasaidia chakula kumeng'enywa vyema kutokana na damu kuwepo katika utumbo mdogo vyema. Ni mkao mgumu kukaa, mwanzoni miguu huwa inakufa ganzi kutokana na kubanwa lakini amini nakwambia ukijilazimisha baada ya muda mfupi maumivu yanaisha kabisa na unaweza kukaa muda mrefu sana bila kuumia kabisa. 

Kuanza meditation

 Ukiwa umeshakaa, kinachofuata ni kuanza meditation. Ukishakaa, relax hakikisha kila kiuongo kimerelax, unganisha mikono yako ubebane pamoja, hisi upendo mwilini mwako, shukuru kwa afya uliyonayo, shukuru kwa jinsi mwili unavyokulindia roho yako iliyohifadhiwa na mwili, hisi furaha, peace, and love within. Halafu vuta pumzi kubwa tano. Vuta pumzi ndani taaaaratibu, halafu pause kidogo then toa pumzi njee TAARATIBU TENA. Wakati huo weka mawazo kwenye pumzi. Baada ya kuvuta pumzi kubwa tano endelea kuvuta pumzi kikawaida huku ukiweka akili kwenye pumzi inavyoingia na kutoka. 
Unaweka akili kwenye pumzi kwa lengo la kutoweka akili kwenye mawazo. Akili ya mwanadamu haiwezi kukaa bila mawazo. Unapomeditate unaweka wazo kwenye pumzi tu, unaangalia jinsi pumzi inavyoingia na kutoka na kufeel energy inayoingia na kutoka mwilini. Uwe umefunga macho. 

Ni vigumu kwa mara za mwanzo kwa sababu, ni vigumu kutuliza akili katika wazo moja kwa muda mrefu ila we jitahidi kufocus kwenye pumzi tu. Baada ya muda, wakati hauwazi wala haufuati kinachokuja akilini ukiwa unaweka mawazo yako katika kutazama tu jinsi pumzi inavyoingia na kutoka mwilini utaanza kuhisi umeme unakuzunguka mwilini, au kichwa kinakuwa kizito, au umeme unapanda na kushuka kwenye uti wa mgongo na utaanza kuhisi mwili mzima umerelax, hapo utakuwa katika hisia ya meditation. Ni hisia nzuri maana zinakufanya unarelax na mwili unajitengenezea umeme wake.






0 Comments

Type and hit Enter to search

Close