Breaking News

Maswali Ya Muhimu Katika Kufahamu Maana Ya Yoga na Meditation

Yoga ni nini?

Neno Yoga limetoka katika linga ya Sanskrit katika neno "Yuj" likiwa na maana ya "kuunganisha" au "muungano". Mwanaume anayefanya Yoga anaitwa Yogi na mwanamke anayefanya Yoga anaitwa Yogini.

Katika historia imeonekana kuwa Yoga ni kitendo ambacho kina historia katika imani za Mashariki hasa katika maandishi, tamaduni na elimu katika jamii ya kale ya Indus. Takribani zaidi ya miaka 3300 Kabla ya Yesu watu walikuwa wanajifunza meditation kwa lengo la kukuza ujuzi wa kiimani. Katika maandashi ya kale sana ya kihindi kuna Sutras. Sutras ni mikao 195 ya Yoga ambayo ilikuwa inatumika hapo kale.
Watu wengi wamekuwa wakiangalia nje yao kutafuta furaha, nguvu, raha, tamaa n.k lakini imekuwa ni vigumu mtu kijiangalia ndani na kutafuta ukweli ndani yake. Pia katika saikolojia imekuwa shida sana kwa watu kujifunza kujiongoza, wengi wamekuwa wakijiongoza kwa kufuata instict, mawazo, hormones na emotions ambazo zinawatawala. Mfano mzuri ni jinsi ya kufanya maamuzi magumu hasa pale inapotokana na mazoea uliyojiwekea. 

Moja ya dhumuni kubwa la Yoga ni kuweza kurudisha ufahamu wako ndani mwako na kuweza kuunganisha mwili na akili kwa pamoja (Kumbuka katika yoga unatakiwa kuweka akili yote kwenye pumzi na energy ya mwili). Mwili na akili pale vinapoweza kukutana unaweza kufanya maamuzi utakayo na unakuwa kiongozi wa maamuzi yako na kiongozi wa mawazo yako. Pia unajifunza kuwa na furaha ya ndani, furaha ambayo haitegemei maisha, mali, hali, watu, au vitu vya nje bali ni furaha ya ndani, furaha isiyoweza kuibiwa na furaha ambayo ni ya milele.




Kwa kufanya yoga, kuweka adabu na umakini katika kila mkao unaongeza concetration, ufahamu, na willing power. Pia kwa kutumia meditation unaongeza ufahamu wa kujitambua na kutambua ufahamu mkuu wa ulimwengu ambao aina zote za ufahamu zimetoka kwake na zipo ndani yake. 

Neno lenyewe "Muunganiko" ni muunganiko kati ya mwili na akili, ufahamu wako na ufahamu wa kuu kaisa,roho na akili.

Hatha ni nini?

Hatha maana yake ni umakini au nia makini. Ni neno linalotumika kumaanisha aina ya mazoezi (asana) ambayo ni maalum kwa ngozi, misuli na mifupa. Na pia aina hizi za mazoezi na mikao ni maalum katika kufungua channel za mwili kutoka katika channel kuu ambayo ni Uti wa mgongo. 

Hatha inamaanisha pia kubalance au kuweka sawa. Ni mikao inayoweka sawa hali zote za balance ya mwili na akili. Ni mikao maalum sana kwani katika historia imepelekea aina mbalimbali ya watu kuweza kujitambua na kuongeza ufahamu wao kutokana na faida zake. Mikao hii tangu miaka ya kale maeneo ya jamii za Kihindi na Asia zimekuwa zikitumiana imezijaribu kwa miaka na miaka na zikaonekana ni kweli zinasaidia na ni muhimu. 


Om ni nini?

Wengi wanafahamu sauti hii ya "Om" ni sauti ambayo inatajwa taaratibu kama "Ohhmmmm". Ni aina ya Mantra (Neno ambalo katika kulirudiarudia unaongeza concentration). Neno hili hutamkwa mwanzo wa Yoga au meditation kwa taaratibu na kwa kuelekeza akili na ufahamu katika sauti yake. Pia ni neno ambalo ulitamkapo kwa utaratibu na umakini unaongeza umakini na amani.

Tangu kale ni neno ambalo inaaminika likitajwa lina sauti sawa na Vibration ya uimwengu, Vibration/mtetemeko au mawimbi ya sauti yake ni sawa na mawambi ya ulimwengu au vibration ya ulimwengu. Imekuja kithibitika hivi juzi katika SAYANSI kuwa ulimwengu ni vibration na katika vibration hiyo inashikilia kila matter na energy. Vibration hiyo imeonekana haina utofauti na sauti ya "Ommm". Kupitia Vibration hiyo kila object ina shape, vibrate, na kuchange katika forms mbalimbali. 

Katika yoga kutaja mantra hiyo ni kujikumbusha kuwa Ulimwengu upo ndani yangu, na mimi ni sehemu ya ulimwengu iliyojitambua. Pia inakupa hisia ya kuwa kila kitu ulimwenguni ni vibration, na pia katika kuchant Omm unajirudhisha katika chanzo kikuu cha uumbaji ambacho kila kitu ni vibration na kila kitu kinasogea taaratibu kwa amani. Kupitia ufahamu wetu, pumzi, na nguvu ya mwili huungana na kutuweka sisi katika ufahamu mkuu. 

 Ninapaswa kufanya Yoga mara ngapi?

Yoga ni tofauti kabisa na vitendo vingine ambavyo tumevizoea kwani katika Yoga unaweza kufanya Yoga mara moja tu kwa wiki na ukaona faida yake. Na ukiweza kufanya zaidi ya hapo bado utaona faida na umuhimu wake. Tafuta muda maalum na jifunze taaratibu na mwishowe utafurahi kuona amani, furaha, umakini, uwezo mzuri wa kufanya maamuzi na kuweza kuongoza mawazo na akili yako. 


Tofauti kati ya Yoga na aina nyingine za mazoezi

Tofauti kuu kati ya Yoga na aina nyingine za mazoezi ni kuwa aina nyingine za mazoezi zinalenga kuongeza nguvu ya mwili kwa misuli, mifupa na viungo. Lakini yoga inalenga kuunganisha mwili, ufahamu, na akili kwa pamoja. Hivyo ni tofauti kabisa na aina nyingine za mazoezi kwani huunganisha nguvu ya mwili, akili na ufahamu kwa pamoja. 

Yoga ni dini? Au ni sehemu ya dini?

Hapana, Yoga sio dini. Mtu yeyote mwenye imani yoyote anaweza kujifunza yoga. Japokuwa Yoga imeanzia katika imani na katika kujifunza kujitambua pia inaweza kutumika na imani yoyote kwani haina sala, au kuabudu au chochote ambacho imani/dini inataka. Ni kuweka akili yako katika mwili kwa ufahamu wako. Hivyo haihusiki na udini. Yoyote anayependa kuondoa msongo wa mawazo, kujitambua, kuwa na amani, kuongeza uwezo wa kujiongoza na kuongoza akili na mawazo anaweza kujifunza. 


Nini kinahitajika ninapotaka nianze Yoga?

Hakuna kinachohitajika zaidi ya Ufahamu wako, akili, na mwili. Vitu vingine vya ziada ni kama vile Yoga Mat (Mkeka wa yoga), T Shirt, suruali au nguo yoyote ya kujisitiri na nyepesi ambayo unaweza kuitumia hata kwa mazoezi. Pia na sehemu tulivu na mwalimu au kitabu cha kukuelekeza. Unaweza kuanza na mkao mmoja ukauzoea na ukaweza kufanya mikao 10 na mpaka zaidi. Cha msingi ni kuanza taaratibu na kuweka nia.


Haya mdau wa mazoezini niachie maoni yako hapo chini kuhusu makala hii uliyoisoma 

0 Comments

Type and hit Enter to search

Close