Breaking News

Faida ya sanaa ya yoga - sensei FUNDI

Mwalimu wa Yoga wa kimataifa,Sensei Rumadha Fundi katika mazoezi tofauti ya sanaa ya Yoga, akielezea ni nini hasa maana ya kutafakari kwa njia ya sanaa ya Yoga.

Meditation & Mantra -- Mara nyingi neno "Meditation" au kutafakari huchanganywa na kufikiri ni kukaa kimya kufumba macho kiufanisi au kuwaza jambo fulani. Pia, wengine huchanganya hili neno na kuwa umekaa kimya na kujaribu kutofikiria lolote, ama pia kuivuta au kuisukuma akili yako na kutoku fikiria kitu cha iana yeyote ile muda wote wa kutafakari na kuamini kwamba hiyo ni “Meditation” au Tafakari. Kamwe, hamna hata moja ya mifano hii inaweza kuifikia maana yake halisi katika mfumo kisayansi na filosofia ya “Yogic”.

Kisayansi ya Yoga, “Meditation” inaitwa “Mtiririko wa akili”(Flow of the mind).” Kuiongoza akili au mawazo ya mtu kupia Meditation, inahitaji pointi au sehemu muhimu katika maungo yako unayo kuwa unatumia kama vile mfano wa mionzi ya akili kuirushia na kuelekeza katika sehemu moja tu. Hivyo kwa kutumia msaada wa sauti maalum itwayo “Mantra”, hiyo ndio chombo hutumika kupitia mkufunzi aliye hitimu Sanaa ya Yoga na kufundisha kutokana na mazingira tofauti kati ya tofauti za watu zilivyo.

Kama jinsi inavyoelezwa katika filosofia ya Yoga kwamba, akili ya mwana adam, kamwe haitulii, wakati wote ipo mbio na inatafuta cha kufikiri, hivyo basi huwa ni kazi ngumu sana kwa mtu hata kuanza tu somo la kwanza (First lesson), kwa mistuko ya mchanganyiko wa mawazo ya mwana adam. Hivyo huwa taabu sana kukusanya mawazo yako binafsi na kufanya meditation bila muongozo wa kiutaam.

Napenda kuongelea vitu vichache hapa. Kuna vitu, au pointi tano tofauti zilizo muhimu na utumika katika mbinu za kutafakari kwa jina la “Sense withdrawal”, ambayo huitajika ili uweze kushawishi akili yako na mawazo kwamba utaweza kutafakari bila vikwazo vya mawzo yoyote au kuwa na utata katika mfomo mzima wa kutafakari. Ufuatao ni muktasari tu wa jinsi gani wana-Yoga wana tafakari kwa masaa mengi bila mgongano au (interruption) kupitia njia hii:

  1. Asana (Mkao wa mazoezi ya Yoga): “Lotus posture” kukunja miguu. Faida zake; kuweza kumiliki viungo vya mwili wakati wa kutafakari. Ndipo jinsi unaweza kumiliki viungo vya mwili wako vinavyokuwezasha kuona vitu “Sensory organs”. Kufumba macho, kutokuona kinachoendelea nje ya upeo wa macho ili kuweza kuelekeza mionzi ya fikra zako (Focus) sehemu moja tu. Kukunja ulimi zidi ya dari ya mdomo “Roof of the mouth” (Palate) wako ili kuweza miliki hamu ya kuonja radha au haja ya chakula chochote kile (Control taste). Kukunja mikono na vidole kuweza kumiliki hamu ya kushika kitu (Control sense of touch). Kitu kisicho wezekana kukimiliki ni harufu (Sense of smell), na ndio maana “Meditation” hufanywa katika mazingira safi bila moshi wala harufu mbaya kuepuka mkatiko wa mtiririko wa mawazo waka wa kutafakari.

  2. Kutoka katika mazingira ya mzumguuko wako wa kila siku (Withdrawal from external world) “Bhuta Shuddhi”. Kujitoa kimawazo kiuwoga wa matatizo ya kila siku kimaisha, kuwa umetulia mwili wako wakati wa kutafakari (Relaxation).

  3. Kujitoa kimawazo katika mwili wako mwenyewe (Withdrawal from the body) “Asana Shuddhi”. Kutowaza lolote kuhusu mwili wako na hali yake nzima au kutokuambatanisha fikra zako katika maumbile ya mwili wako (Withdrawal from each parts of your body; concentrate in one singular point) “Ista Chakra”.

  4. Kujitoa kabisa kimawazo (Withdrawal from thoughts of interruption) “Citta Shuddhi”, hapa katika hatua hii, mraba wa akili unakuwa unaelea kimawazo sambamba katika anga za ulimwengu (Total suspension of mind in cosmic space; Consciousness)

  5. Mtiririko wa mawazo na Mantra (Flow of mind) “Dhyana” hii ndio njia nzima ya utaratibu wa kufanya Meditation, au kwa namna nyingine ni mwanzo wa Kutafakari (Process to start meditating). Hapa ndipo sasa mkufunzi wa taaluma ya Yoga anakuwa anarudia kimoyo moyo Mantra aliyoisoma, sasa hapa ndipo mwanzo wa kile tunaita “Tafakari”. (Meditation).
Zipo njia nyingi zaidi za kufanya “Meditation” au kutafakari ngazi ya juu zaidi kupitia njia ya pumzi au “Prana Yama”(Vital Breathing). Hivyo, huu hapa ni muktasari tu wa jinsi na namna gani tunaitafsiri “Meditation ” au kutafakari kupitia mafunzo ya Yoga. Hayo pia ni machache naona vizuri kushirikiana na kumulika mwanga kidogo kwa wale wasio fahamu nini hasa maana ya Meditation kupitia Sanaa yaYoga.


  • Imeandikwa na mkufunzi wa Sanaa ya Yoga, Rumadha Fundi, mwenye uzoefu mkubwa na diploma ya somo la Yoga toka “ College of Neo-humanists Studies, Gullringen, Vimmerby, Sweden, aliyopa mwaka 1986 na hatimae baadae mwaka 1987 kwenda Tiljala, Culcutta, India, na kupata shahada ya juu kabisa ya Yoga duniani ijulikanayo kwa jina la “Avadhuta”.

0 Comments

Type and hit Enter to search

Close